Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 3:5 - Swahili Revised Union Version

5 Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema nitapambana nawe; nitalipandisha vazi lako hadi kichwani, niyaache mataifa yauone uchi wako, tawala ziikodolee macho aibu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anasema, “Mimi ni kinyume na ninyi. Nitafunika uso wako kwa gauni lako. Nitaonesha mataifa uchi wako na falme aibu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 bwana Mwenye Nguvu Zote anasema, “Mimi ni kinyume na ninyi. Nitafunika uso wako kwa gauni lako. Nitaonyesha mataifa uchi wako na falme aibu yako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi; nami nitayainua marinda yako mbele ya uso wako; nami nitawaonesha mataifa uchi wako, na falme aibu yako.

Tazama sura Nakili




Nahumu 3:5
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe ukisema moyoni mwako, Mbona mambo haya yamenipata mimi? Ni kwa sababu ya wingi wa uovu wako, marinda yako yamefunuliwa, na visigino vya miguu yako vimeumia.


Kwa ajili ya hayo, mimi nami nitayafunua marinda yako mbele ya uso wako, na aibu yako itaonekana.


Tazama, mimi ni juu yako, Ewe mwenye kiburi, asema Bwana, BWANA wa majeshi; maana siku yako imewadia, wakati nitakapokujia.


basi, tazama, nitawakusanya wapenzi wako wote ambao umejifurahisha pamoja nao, nao wote uliowapenda, pamoja na watu wote uliowachukia; naam, nitawakusanya juu yako pande zote, na kuwafunulia uchi wako, wapate kuuona uchi wako wote.


uiambie nchi ya Israeli, BWANA asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, nami nitautoa upanga wangu alani, nami nitamkatilia mbali nawe mtu mwenye haki na mtu mbaya.


Nami nitaweka wivu wangu juu yako, nao watakutenda mambo kwa ghadhabu; watakuondolea pua yako na masikio yako; na mabaki yako wataanguka kwa upanga; watawatwaa wanao na binti zako; na mabaki yako watateketea motoni.


nao watakutenda mambo kwa chuki, watakunyang'anya matunda yote ya kazi yako, watakuacha uchi, huna nguo na aibu ya mambo yako ya kikahaba itafunuliwa, uasherati wako na uzinzi wako.


basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi kupigana nawe, kama bahari iinuavyo mawimbi yake.


Piteni; njia yenu, wakazi wa Shafiri, mkiwa uchi na wenye aibu; Wakazi wa Saanani msitokeze nje; Beth-eseli unalia na ataondoa msaada wake kwenu;


Tazama, mimi ni juu yako, asema BWANA wa majeshi, nami nitayateketeza magari yako ya vita katika moshi, na upanga utawaangamiza wanasimba wako; nami nitayakatilia mbali mawindo yako katika nchi, na sauti za wajumbe wako hazitasikiwa tena kamwe.


Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kulia wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo