Methali 9:6 - Swahili Revised Union Version Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.” Biblia Habari Njema - BHND Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Achana na ujinga upate kuishi; fuata njia ya akili.” Neno: Bibilia Takatifu Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. Neno: Maandiko Matakatifu Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu. BIBLIA KISWAHILI Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu. |
ili waende katika amri zangu, na kuyashika maagizo yangu, na kuyatenda; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Na mtumishi wangu, Daudi, atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja; nao watayafuata maagizo yangu, na kuzishika amri zangu, na kuzitenda.
Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze.
Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.