Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 18:4 - Swahili Revised Union Version

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema, “Watu wangu, ondokeni kwake, ili msishirikiane naye katika dhambi zake, msije mkaipata adhabu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “ ‘Tokeni katikati yake, enyi watu wangu,’ ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni ikisema: “Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lolote;

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 18:4
16 Marejeleo ya Msalaba  

Lutu akatoka na kusema na wachumba wa binti zake, akawaambia, “Ondokeni mahali hapa kwa sababu BWANA atauharibu mji huu”. Lakini akaonekana kama achezaye machoni pa wakwe zake.


Ulipomwona mwizi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi.


Haya, tokeni katika Babeli, Kimbieni kutoka kwa Wakaldayo; Hubirini kwa sauti ya kuimba, tangazeni haya, Yatamkeni mpaka mwisho wa dunia, semeni, BWANA amemkomboa mtumishi wake, Yakobo.


Nendeni zenu, nendeni zenu, tokeni huko, msiguse kitu kichafu; tokeni kati yake; iweni safi ninyi mnaochukua vyombo vya BWANA.


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, mkatoke katika nchi ya Wakaldayo, mkawe kama mabeberu mbele ya makundi.


Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka kwa hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu.


Ninyi mliojiepusha na upanga, Nendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.


Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo.


Tungependa kuuponya Babeli, Lakini haukuponyeka; Mwacheni, nasi twendeni zetu, Kila mtu hata nchi yake mwenyewe; Maana hukumu yake inafika hata mbinguni, Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.


na kusema, Kama sisi tungalikuwako zamani za baba zetu, hatungalishirikiana nao katika damu ya manabii.


Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.


Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usizishiriki dhambi za watu wengine. Ujilinde nafsi yako uwe safi.


Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo