Methali 9:12 - Swahili Revised Union Version Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara. Biblia Habari Njema - BHND Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama una hekima, itakufaa wewe mwenyewe; kama ukiidharau, mwenyewe utapata hasara. Neno: Bibilia Takatifu Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” Neno: Maandiko Matakatifu Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.” BIBLIA KISWAHILI Kama una hekima, una hekima kwa nafsi yako; Na kama una dharau, utaichukua peke yako. |
Basi sasa msiwe watu wenye kudharau, vifungo vyenu msije vikakazwa; maana nimesikia kwa Bwana, BWANA wa majeshi, habari ya hukumu itakayotimizwa, nayo imekusudiwa, itakayoipata dunia yote pia.
Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake.
akisema juu ya mambo haya kama afanyavyo katika barua zake zote pia, katika barua hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuyaelewa na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wapotoavyo Maandiko mengine, na kujiletea maangamizi wao wenyewe.