Methali 8:9 - Swahili Revised Union Version Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi, kwa mwenye maarifa yote ni sawa. Biblia Habari Njema - BHND Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi, kwa mwenye maarifa yote ni sawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa mtu mwelewa kila kitu ni wazi, kwa mwenye maarifa yote ni sawa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa wenye kupambanua, yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa wenye kupambanua yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa. BIBLIA KISWAHILI Yote humwelea yule afahamuye, Yote huelekea mbele yao waliopata maarifa. |
Hekima huwa machoni pake mwenye ufahamu; Bali macho ya mpumbavu huwa katika ncha za dunia.
Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
Je! Litasemwa neno hili, enyi nyumba ya Yakobo, Roho ya BWANA imepunguzwa? Je! Haya ni matendo yake? Je! Maneno yangu hayamfai yeye aendaye kwa unyofu?
Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.
Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua habari ya yale mafunzo, kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.