Methali 8:7 - Swahili Revised Union Version Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kinywa changu kitatamka kweli tupu; uovu ni chukizo midomoni mwangu. Biblia Habari Njema - BHND Kinywa changu kitatamka kweli tupu; uovu ni chukizo midomoni mwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kinywa changu kitatamka kweli tupu; uovu ni chukizo midomoni mwangu. Neno: Bibilia Takatifu Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu. Neno: Maandiko Matakatifu Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu. BIBLIA KISWAHILI Maana kinywa changu kitasema kweli, Na uovu ni chukizo kwa midomo yangu. |
Mtu aliye dhalimu ni chukizo kwa wenye haki; Na mnyofu wa mwenendo ni chukizo kwa waovu.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Basi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme basi? Yesu akajibu, Wewe wasema, kwa kuwa mimi ni mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Kila aliye wa hiyo kweli hunisikia sauti yangu.
Yesu akajibu, akawaambia, Mimi ningawa ninajishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ndio kweli; kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka wala niendako.
Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Laodikia andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye Amina, Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli, mwanzo wa kuumba kwa Mungu.