Methali 3:1 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu, bali kwa moyo wako uzishike amri zangu. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako, BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu. |
Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea; Umtafute mtumishi wako; Kwa maana sikuyasahau maagizo yako.
Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.
Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la BWANA, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu chochote ulichokatazwa na BWANA, Mungu wenu,
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;
Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Amri hii ninayokuamuru leo mtaizingatia, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki.