Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.
Methali 24:23 - Swahili Revised Union Version Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Biblia Habari Njema - BHND Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ifuatayo pia ni misemo ya wenye hekima: Kupendelea watu katika hukumu si vizuri. Neno: Bibilia Takatifu Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonesha upendeleo katika hukumu si vyema: Neno: Maandiko Matakatifu Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonyesha upendeleo katika hukumu si vyema: BIBLIA KISWAHILI Haya nayo pia ni maneno ya wenye akili. Kupendelea watu katika hukumu si kwema. |
Basi sasa hofu ya BWANA na iwe juu yenu; aiweni waangalifu katika jambo mtendalo, kwa maana kwa BWANA, Mungu wetu hakuna upotoshaji wala kupendelea nafsi za watu au kupokea rushwa.
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu;
Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.
Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Msitazame nafsi za watu katika hukumu; muwasikize wadogo na wakubwa sawasawa; msiche uso wa mtu yeyote; kwa kuwa hukumu ni ya Mungu; na lile neno liwashindalo mniletee mimi, nami nitalisikiza.
Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.
Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.
Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, nendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni.