Methali 24:2 - Swahili Revised Union Version Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao. Biblia Habari Njema - BHND maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana fikira zao zote ni juu ya ukatili, hamna jema lolote litokalo midomoni mwao. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema kuhusu kuleta madhara. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema juu ya kuleta madhara. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana moyo wao hufikiri dhuluma, Na midomo yao huongea madhara. |
Kinywa chake kimejaa laana, Na hila na dhuluma. Chini ya ulimi wake kuna madhara na uovu,
Usinikokote pamoja na wasio haki, Wala pamoja na watenda maovu. Wawaambiao jirani zao maneno ya amani, Lakini mioyoni mwao mna madhara.
Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.
Basi kwa ajili ya hayo Mtakatifu wa Israeli asema hivi, Kwa sababu mwalidharau neno hili, na kutumainia jeuri na ukaidi, na kuyategemea hayo;
Hakuna anayeshitaki kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.
Mikono yao ni hodari kwa kutenda maovu; afisa na hakimu wanataka rushwa, mtu mkubwa hunena madhara yaliyomo rohoni mwake; hivyo ndivyo wayafumavyo hayo pamoja.
akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?
Naye Daudi alifahamu ya kuwa Sauli amemkusudia mabaya; akamwambia Abiathari, kuhani, Lete hapa hiyo naivera.