Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Matendo 13:10 - Swahili Revised Union Version

10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 akasema, “Mdanganyifu wa kupindukia na mlaghai wewe! Wewe ni mtoto wa Ibilisi! Wewe ni adui wa chochote kile kilicho cha kweli; hukomi hata mara moja kujaribu kuzipotosha njia za Bwana zilizonyoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Mwenyezi Mungu zilizo nyoofu?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Mwenyezi Mungu zilizonyooka?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyooka?

Tazama sura Nakili




Matendo 13:10
23 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana nimemchagua ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.


nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.


Ukainuliwa moyo wake katika njia za BWANA; na zaidi ya hayo akapaondoa mahali pa juu, na Maashera, katika Yuda.


Baa hilo ni katika mambo yote yanayofanyika chini ya jua, ya kuwa wote wanalo tukio moja; naam, zaidi ya hayo, mioyo ya wanadamu imejaa maovu, na wazimu umo mioyoni mwao wakati walipo hai, na baadaye huenda kwa wafu.


Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu.


Ni nani aliye na hekima, naye atayafahamu mambo haya? Ni nani aliye na busara, naye atayajua? Kwa maana njia za BWANA zimenyoka, nao wenye haki watakwenda katika njia hizo; bali waasio wataanguka ndani yake.


lile shamba ni ulimwengu; zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;


Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;


Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnawafungia watu ufalme wa mbinguni; ninyi wenyewe hamwingii, wala wanaoingia hamwaachi waingie.


Na alipoona wengi miongoni mwa Mafarisayo na Masadukayo wakiujia ubatizo wake, aliwaambia, Enyi wazawa wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia hasira itakayokuja?


Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang'anyi na uovu.


Ole wenu, enyi wanasheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.


Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.


Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo; wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hamna hiyo kweli ndani yake. Asemapo uongo, husema yaliyo yake mwenyewe; kwa sababu yeye ni mwongo, na baba wa uongo.


tena katika ninyi wenyewe watainuka watu wakisema mapotovu, wawavute hao wanafunzi wawafuatie wao.


Lakini nahofu; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.


Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza Injili ya Kristo.


ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa mafundisho, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.


wakiiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaamu, mwana wa Beori, aliyependa ujira wa udhalimu;


atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo