Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Methali 23:29 - Swahili Revised Union Version Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi? Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Biblia Habari Njema - BHND Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi? Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi? Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Neno: Bibilia Takatifu Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu? Neno: Maandiko Matakatifu Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu? BIBLIA KISWAHILI Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? |
Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.
Naye Daudi akamwalika, akala, akanywa mbele yake; naye akamlevya; hadi wakati wa jioni akatoka kwenda kulala kitandani mwake pamoja na watumishi wa bwana wake, lakini hakushuka nyumbani kwake.
Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.
Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!