Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Methali 23:30 - Swahili Revised Union Version

30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Ni hao wanaokaa sana kwenye mvinyo, hao wanaoenda kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.

Tazama sura Nakili




Methali 23:30
10 Marejeleo ya Msalaba  

akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.


Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.


Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.


Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.


Amechinja nyama zake, amechanganya divai yake, Ameiandalia meza yake pia.


Lakini hawa nao wamekosa kwa divai, wamepotea kwa kileo; kuhani na nabii wamekosa kwa kileo, wamemezwa kwa divai, wamepotea kwa kileo; hukosa katika maono, hujikwaa katika hukumu.


Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!


ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu.


Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;


Kisha Abigaili alimjia Nabali; na tazama, alikuwa amefanya karamu nyumbani mwake, kama karamu ya kifalme; na moyo wake huyo Nabali ukafurahiwa ndani yake, kwa maana amelewa kabisa. Kwa sababu hiyo hakumwambia neno, dogo wala kubwa, hadi kulipopambazuka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo