Methali 22:4 - Swahili Revised Union Version Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu, utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai. Biblia Habari Njema - BHND Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu, utapata tuzo: Fanaka, heshima na uhai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukinyenyekea na kumcha Mwenyezi-Mungu, utapata tuzo: fanaka, heshima na uhai. Neno: Bibilia Takatifu Unyenyekevu na kumcha Mwenyezi Mungu huleta utajiri, heshima na uzima. Neno: Maandiko Matakatifu Unyenyekevu na kumcha bwana huleta utajiri, heshima na uzima. BIBLIA KISWAHILI Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha BWANA Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima. |
Kuna hazina ya thamani na mafuta katika maskani ya mwenye hekima; Bali mwanadamu aliye mpumbavu huyameza.
Miiba na mitego huwa katika njia ya mshupavu; Yeye aitunzaye nafsi yake atakuwa mbali nayo.
Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Nyakati zako zitakuwa nyakati za kukaa imara; za wokovu tele na hekima na maarifa; kumcha BWANA ni hazina yake ya akiba.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Basi wakati huo huo fahamu zangu zikanirudia, na kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu, enzi yangu na fahari yangu zikanirudia; na mawaziri wangu, na madiwani wangu, wakaja kunitafuta; nami nikathibitika katika ufalme wangu, nikaongezewa enzi kupita kiasi.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.