mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Methali 21:11 - Swahili Revised Union Version Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima; Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima; ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa. Biblia Habari Njema - BHND Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima; ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima; ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa. Neno: Bibilia Takatifu Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima anafundishwa, hupata maarifa. Neno: Maandiko Matakatifu Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima afundishwapo, hupata maarifa. BIBLIA KISWAHILI Mwenye mzaha aadhibiwapo, mjinga hupata hekima; Na mwenye hekima afundishwapo, hupokea maarifa. |
mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.
Mpige mwenye mzaha, na mjinga atapata busara; Mwonye mwenye ufahamu, naye atatambua maarifa.
Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
Nao Israeli wote waliokuwa kandokando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi.
Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya.
Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
Na katika saa ile palikuwa na tetemeko kuu la nchi, na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka; wanadamu elfu saba wakauawa katika tetemeko lile. Na waliobakia wakaingiwa na hofu, wakamtukuza Mungu wa mbingu.