Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Methali 20:21 - Swahili Revised Union Version Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni, haitakuwa ya heri mwishoni. Biblia Habari Njema - BHND Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni, haitakuwa ya heri mwishoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni, haitakuwa ya heri mwishoni. Neno: Bibilia Takatifu Urithi upatikanao haraka mwanzoni, hautabarikiwa mwishoni. Neno: Maandiko Matakatifu Urithi upatikanao haraka mwanzoni, hautabarikiwa mwishoni. BIBLIA KISWAHILI Urithi uliopatikana mwanzo kwa haraka, Mwisho wake, lakini, hautabarikiwa. |
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!
Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.
Kama hamtaki kusikia, na kama hamtaki kuitia moyoni, ili kulitukuza jina langu, asema BWANA wa majeshi, basi nitawaleteeni laana, nami nitazilaani baraka zenu; naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamyatii haya moyoni.
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na mtego, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, zinazowaingiza watu katika upotevu na uharibifu.