Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtangomwitu, akayachuma matangomwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasuapasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
Methali 19:2 - Swahili Revised Union Version Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Haifai mtu kuwa bila akili; mwenda harakaharaka hujikwaa. Biblia Habari Njema - BHND Haifai mtu kuwa bila akili; mwenda harakaharaka hujikwaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Haifai mtu kuwa bila akili; mwenda harakaharaka hujikwaa. Neno: Bibilia Takatifu Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. Neno: Maandiko Matakatifu Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia. BIBLIA KISWAHILI Tena si vizuri nafsi ya mtu ikose maarifa; Naye afanyaye haraka kwa miguu hutenda dhambi. |
Na mmoja wao akaenda nje kondeni ili kuchuma mboga, akaona mtangomwitu, akayachuma matangomwitu, hata nguo yake ikawa imejaa, akaja akayapasuapasua sufuriani; kwa maana hawakuyajua.
Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Usitoke nje kwa haraka ili kuyashindania; Usije ukakosa kujua la kutenda hatimaye, Mwenzako atakapokuwa amekuaibisha.
Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele; Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.
Je! Umemwona mtu mwenye kuhamaki katika maneno? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye.
Lakini, kwa sababu huyo Mhubiri alikuwa na hekima, aliendelea kuwafundisha watu maarifa, naam, akatafakari, akachunguza, akatunga mithali nyingi.
Matawi yake yatakapokauka yatavunjwa; wanawake watakuja na kuyachoma moto; kwa maana hawa si watu wenye akili; kwa sababu hiyo yeye aliyewaumba hatawahurumia, yeye aliyewafanya hatawasamehe.
kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;