Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 28:16 - Swahili Revised Union Version

16 kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu: “Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi, jiwe ambalo limethibitika. Jiwe la pembeni, la thamani, jiwe ambalo ni la msingi thabiti; jiwe lililo na maandishi haya: ‘Anayeamini hatatishika.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa hiyo hivi ndivyo bwana Mwenyezi asemavyo: “Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti. Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.

Tazama sura Nakili




Isaya 28:16
25 Marejeleo ya Msalaba  

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli,


Wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda nje katika jangwa la Tekoa; nao walipokuwa wakitoka, Yehoshafati akasimama, akasema, Nisikieni, enyi Yuda nanyi wenyeji wa Yerusalemu; mwaminini BWANA, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.


Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Msingi wake upo Juu ya milima mitakatifu.


Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.


Kwa ajili ya hayo BWANA atangoja, ili awaonee huruma, na kwa ajili ya hayo atatukuzwa, ili awarehemu; kwa maana BWANA ni Mungu wa hukumu; heri wote wamngojao.


Ewe uliyeteswa, uliyerushwa na tufani, usiyetulizwa, tazama, nitaweka mawe yako kwa rangi nzuri, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.


Na kama vile ulivyoona ya kuwa jiwe lilichongwa mlimani bila kazi ya mikono, na ya kuwa lilivunjavunja kile chuma, na ile shaba na ule udongo, na ile fedha, na ile dhahabu; basi Mungu aliye mkuu amemjulisha mfalme mambo yatakayokuwa baadaye; na ndoto hii ni ya hakika, na tafsiri yake ni thabiti.


Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila kamanda.


Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja.


Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni la ajabu machoni petu?


Hata andiko hili hamjalisoma, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika.


kama ilivyoandikwa, Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao; Na kila amwaminiye hatatahayarika.


Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.


Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo