Isaya 28:15 - Swahili Revised Union Version15 Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli; Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema15 “Nyinyi mnajidai mmefanya mkataba na kifo, mmefanya mapatano na Kuzimu! Nyinyi mwasema eti balaa lijapo halitawapata, kwa sababu mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu, na udanganyifu kuwa kinga yenu!” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND15 “Nyinyi mnajidai mmefanya mkataba na kifo, mmefanya mapatano na Kuzimu! Nyinyi mwasema eti balaa lijapo halitawapata, kwa sababu mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu, na udanganyifu kuwa kinga yenu!” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza15 “Nyinyi mnajidai mmefanya mkataba na kifo, mmefanya mapatano na Kuzimu! Nyinyi mwasema eti balaa lijapo halitawapata, kwa sababu mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu, na udanganyifu kuwa kinga yenu!” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu15 Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, tumefanya mapatano na Kuzimu. Pigo linalofurika litakapopita, haliwezi kutugusa sisi, kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu15 Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, tumefanya mapatano na kuzimu. Wakati pigo lifurikalo litakapopita, haliwezi kutugusa sisi, kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.” Tazama sura |
Lakini bila shaka tutalitimiza kila neno lililotoka katika vinywa vyetu, kumfukizia uvumba malkia wa mbinguni, na kummiminia sadaka za kinywaji, kama tulivyotenda sisi, na baba zetu, na wafalme wetu, na wakuu wetu, katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu; maana wakati huo tulikuwa na chakula tele, na kufanikiwa, wala hatukuona mabaya.