Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie.
Methali 16:29 - Swahili Revised Union Version Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Neno: Bibilia Takatifu Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya. Neno: Maandiko Matakatifu Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya. BIBLIA KISWAHILI Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema. |
Kwa sababu hii aliajiriwa, ili mimi niogope, nikafanye hivyo na kutenda dhambi, kisha wao wawe nazo habari mbaya, ili wanishutumie.
Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa.
Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya.
Basi, wapenzi kwa kuwa mmejua hayo, jihadharini msije mkapotoshwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthabiti wenu.
Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.
Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue?