Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na watu wote wa Yuda; basi akawa na mali na heshima tele.
Methali 16:12 - Swahili Revised Union Version Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Biblia Habari Njema - BHND Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Neno: Bibilia Takatifu Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kupitia haki. Neno: Maandiko Matakatifu Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki. BIBLIA KISWAHILI Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. |
Kwa hiyo BWANA akauthibitisha ufalme mkononi mwake; Yehoshafati akaletewa zawadi na watu wote wa Yuda; basi akawa na mali na heshima tele.
Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.
Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.
Kwa kuwa wote wayatendao mambo kama haya, wote watendao yasiyo haki, ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Kisha nikaziona mbingu zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye Mwaminifu na Wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita.