Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Methali 15:30 - Swahili Revised Union Version Mng'ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari njema huuburudisha mwili. Biblia Habari Njema - BHND Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari njema huuburudisha mwili. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari njema huuburudisha mwili. Neno: Bibilia Takatifu Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya. Neno: Maandiko Matakatifu Mtazamo wa tabasamu huleta furaha moyoni, nazo habari njema huipa mifupa afya. BIBLIA KISWAHILI Mng'ao wa macho huufurahisha moyo; Habari njema huinenepesha mifupa. |
Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.
Kama vile maji ya baridi kwa mtu mwenye kiu, Ndivyo ilivyo habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.
Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.