Methali 13:25 - Swahili Revised Union Version Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza, lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa. Biblia Habari Njema - BHND Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza, lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwadilifu anacho chakula cha kumtosheleza, lakini tumbo la waovu hutaabika kwa njaa. Neno: Bibilia Takatifu Mwenye haki hula hadi akaridhisha moyo wake, bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake, bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa. BIBLIA KISWAHILI Mwenye haki hula akaishibisha nafsi yake; Bali tumbo la mtu mbaya litaona njaa. |
Wanasimba hutindikiwa, na kuona njaa; Bali wamtafutao BWANA hawapungukiwi kitu chochote kilicho chema.
BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa.
Alipokuwa amekwisha tumia vyote, njaa kubwa iliingia katika nchi ile, yeye naye akaanza kuhitaji.
kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini.
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.
Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.