Methali 11:21 - Swahili Revised Union Version Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazawa wa wenye haki wataokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa, lakini waadilifu wataokolewa. Biblia Habari Njema - BHND Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa, lakini waadilifu wataokolewa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hakika mwovu hataepa kuadhibiwa, lakini waadilifu wataokolewa. Neno: Bibilia Takatifu Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru. Neno: Maandiko Matakatifu Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa, bali wenye haki watakuwa huru. BIBLIA KISWAHILI Hakika, mtu mwovu hatakosa adhabu; Bali wazao wa wenye haki wataokoka. |
Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;
Jitenge mbali na neno la uongo; wala wasio hatia na wenye haki usiwaue; kwa kuwa mimi sitamhesabia haki yeye aliye mwovu.
Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, Ndivyo alivyo mwanamke mzuri asiye na akili.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Mimi sina hasira ndani yangu; Kama mbigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;
Ndipo watu wote waliojua ya kuwa wake zao waliwafukizia uvumba miungu mingine, na wanawake wote waliosimama karibu, mkutano mkubwa, yaani, watu wote waliokaa katika nchi ya Misri, katika Pathrosi, wakamjibu Yeremia, wakisema,
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.