Methali 10:25 - Swahili Revised Union Version Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kimbunga hupita na mwovu hutoweka, lakini mwadilifu huimarishwa milele. Biblia Habari Njema - BHND Kimbunga hupita na mwovu hutoweka, lakini mwadilifu huimarishwa milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kimbunga hupita na mwovu hutoweka, lakini mwadilifu huimarishwa milele. Neno: Bibilia Takatifu Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele. Neno: Maandiko Matakatifu Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele. BIBLIA KISWAHILI Kisulisuli kikiisha pita asiye haki hayuko tena; Bali mwenye haki ni msingi wa milele. |
Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.
Hofu yenu ifikapo kama tufani, Na msiba wenu ufikapo kama kisulisuli, Dhiki na taabu zitakapowafikia.
Naam, hawakupandwa; hawakutiwa katika ardhi kama mbegu; naam, shina lao halikutia mizizi katika ardhi; tena awapuzia tu, wakanyauka, upepo wa kisulisuli wawaondoa kama mabua makavu.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.