Methali 10:16 - Swahili Revised Union Version Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima; Mazao ya wabaya huielekea dhambi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tuzo la mtu mwema ni uhai, lakini mwovu huishia katika dhambi. Biblia Habari Njema - BHND Tuzo la mtu mwema ni uhai, lakini mwovu huishia katika dhambi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tuzo la mtu mwema ni uhai, lakini mwovu huishia katika dhambi. Neno: Bibilia Takatifu Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu ni dhambi na mauti. Neno: Maandiko Matakatifu Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu huwaletea adhabu. BIBLIA KISWAHILI Kazi yake mwenye haki huuelekea uzima; Mazao ya wabaya huielekea dhambi. |
Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wizi, ushuhuda wa uongo, na matukano;
Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele; ambacho Mwana wa Adamu atawapa, kwa sababu huyo ndiye aliyetiwa mhuri na Baba, yaani, Mungu.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mnajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
Lakini watu waovu na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na kudanganyika.
Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.