Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Methali 1:7 - Swahili Revised Union Version Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Biblia Habari Njema - BHND Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Neno: Bibilia Takatifu Kumcha Mwenyezi Mungu ni chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Neno: Maandiko Matakatifu Kumcha bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. BIBLIA KISWAHILI Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. |
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; Bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.
Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.