Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika shimo mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Methali 1:10 - Swahili Revised Union Version Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi. Biblia Habari Njema - BHND Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi. Neno: Bibilia Takatifu Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. Neno: Maandiko Matakatifu Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. BIBLIA KISWAHILI Mwanangu, wenye dhambi wakikushawishi, Wewe usikubali. |
Haya, twende, tukamwue na kumtupa katika shimo mojawapo, nasi tutasema, Mnyama mkali amemla; kisha tutaona zitakuwaje ndoto zake.
Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
Ni yeye aendaye kwa haki, anenaye maneno ya adili; ni yeye anayedharau faida ipatikanayo kwa dhuluma; akung'utaye mikono yake asipokee rushwa; azibaye masikio yake asisikie habari za umwagaji wa damu; afumbaye macho yake asitazame uovu.
Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu.
usimkubalie wala usimsikize; wala jicho lako lisimwonee huruma, wala usimwache, wala usimfiche;