Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Mathayo 20:2 - Swahili Revised Union Version Naye alipokwisha kupatana na wafanya kazi kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akapatana nao kuwalipa fedha denari moja kwa siku, kisha akawapeleka katika shamba lake la mizabibu. Biblia Habari Njema - BHND Akapatana nao kuwalipa fedha denari moja kwa siku, kisha akawapeleka katika shamba lake la mizabibu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akapatana nao kuwalipa fedha denari moja kwa siku, kisha akawapeleka katika shamba lake la mizabibu. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu. BIBLIA KISWAHILI Naye alipokwisha kupatana na wafanya kazi kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. |
Na itakuwa, mara mimi nikiondoka kwako, Roho ya BWANA atakuchukua uende nisikojua; nami nitakapokwenda kumwambia Ahabu, naye asipokuona, ataniua, lakini mimi mtumishi wako namcha BWANA tangu ujana wangu.
Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akiwa bado mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa Maashera, na sanamu za kuchonga, na za kusubu.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa.
Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyetoka alfajiri kwenda kuwaajiri wafanya kazi awapeleke katika shamba lake la mizabibu.
Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.
Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye.
Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.
Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana aliyevaa naivera ya kitani.
Basi, mtoto Samweli akamtumikia BWANA mbele ya Eli. Na neno la BWANA lilikuwa adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.
Naye BWANA akaonekana tena huko Shilo; kwa kuwa BWANA akajifunua kwa Samweli huko Shilo, kwa neno la BWANA. Nalo neno la Samweli likawajia Israeli wote.