Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Marko 12:15 - Swahili Revised Union Version

15 Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini Yesu alijua unafiki wao, akawaambia, “Mbona mnanijaribu? Nionesheni hiyo sarafu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Isa alijua unafiki wao. Akawauliza, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Isa alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Tumpe, tusimpe? Naye, akijua unafiki wao, akawaambia, Mbona mmenijaribu? Nileteeni dinari niione.

Tazama sura Nakili




Marko 12:15
14 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli mithali;


Naye alipokwisha kupatana na wafanya kazi kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu.


Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?


Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe? Huku wakimjaribu.


Hata walipofika walimwambia, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu; lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu. Je! Ni halali kumpa Kaisari kodi au siyo?


Wakaileta. Akawaambia, Ni ya nani sanamu hii na anwani hii? Wakamwambia, Ni ya Kaisari.


Lakini yeye alitambua hila yao, akawaambia,


Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda? Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.


Nao wakasema neno hilo wakimjaribu, ili wapate sababu ya kumshitaki. Lakini Yesu akainama, akaandika kwa kidole chake katika ardhi.


Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.


Wala tusimjaribu Bwana, kama wengine wao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka.


Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.


nami nitawaua watoto wake kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye fikira na mioyo. Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo