Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
Mathayo 14:11 - Swahili Revised Union Version Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule msichana; akakileta kwa mamaye. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake. Biblia Habari Njema - BHND Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake. Neno: Bibilia Takatifu Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. Neno: Maandiko Matakatifu Kichwa chake kikaletwa kwenye sinia, akapewa yule binti, naye akampelekea mama yake. BIBLIA KISWAHILI Kichwa chake kikaletwa katika kombe, akapewa yule msichana; akakileta kwa mamaye. |
Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
Bali macho yako na moyo wako hauna utakalo ila kutamani, na kumwaga damu isiyo na hatia, na kudhulumu, na kutenda jeuri.
Basi, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, nitakuweka tayari kwa damu, na damu itakufuatia; ikiwa hukuchukia damu, basi damu itakufuatia.
Wanafunzi wake wakaenda, wakamchukua yule maiti, wakamzika; kisha wakaenda wakampasha Yesu habari.
Naye, huku akichochewa na mamaye, akasema, Nipe hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.
kwa kuwa walimwaga damu ya watakatifu na ya manabii, nawe umewapa damu wainywe; ndiyo wanayostahili.
Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu sana.