Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
Marko 3:22 - Swahili Revised Union Version Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.” Biblia Habari Njema - BHND Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.” Neno: Bibilia Takatifu Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa nguvu ya mkuu wa pepo wachafu!” Neno: Maandiko Matakatifu Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!” BIBLIA KISWAHILI Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo. |
Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.
Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake,
Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.
Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?
Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.