Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Marko 3:22 - Swahili Revised Union Version

22 Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Nao waalimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu, wakasema, “Ana Beelzebuli! Tena, anawafukuza pepo kwa nguvu ya mkuu wa pepo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa nguvu ya mkuu wa pepo wachafu!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa kutumia mkuu wa pepo wachafu!”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Nao waandishi walioshuka kutoka Yerusalemu wakasema, Ana Beelzebuli, na, Kwa mkuu wa pepo huwatoa pepo.

Tazama sura Nakili




Marko 3:22
14 Marejeleo ya Msalaba  

Na Ahazia akaanguka kutoka dirisha la chumba chake ghorofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Nendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona ugonjwa huu.


Lakini mimi ni mdudu wala si mtu, Nimedharauliwa na kupuuzwa na watu.


Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?


Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo.


Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.


Ndipo Mafarisayo na waandishi toka Yerusalemu walipomwendea Yesu wakisema,


Lakini Mafarisayo wakasema, Kwa nguvu za mkuu wa pepo atoa pepo.


Kisha Mafarisayo, na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemu, wakakusanyika mbele yake,


Wengine wao wakasema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo.


Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Yudea, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.


Basi huko Yerusalemu ilikuwa sikukuu ya kutabaruku; ni wakati wa baridi.


Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua?


Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?


Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo