Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Isaya 28:6 - Swahili Revised Union Version Naye atakuwa roho ya hukumu ya haki kwake yeye aketiye ili ahukumu; naye atakuwa nguvu kwao walindao langoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waamuzi mahakamani atawaongoza kutenda haki, nao walinzi wa mji atawapa nguvu. Biblia Habari Njema - BHND Waamuzi mahakamani atawaongoza kutenda haki, nao walinzi wa mji atawapa nguvu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waamuzi mahakamani atawaongoza kutenda haki, nao walinzi wa mji atawapa nguvu. Neno: Bibilia Takatifu Atakuwa roho ya haki kwa yeye anayeketi kwenye kiti cha hukumu, chanzo cha nguvu kwa wale wazuiao vita langoni. Neno: Maandiko Matakatifu Atakuwa roho ya haki kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu, chanzo cha nguvu kwa wale wazuiao vita langoni. BIBLIA KISWAHILI Naye atakuwa roho ya hukumu ya haki kwake yeye aketiye ili ahukumu; naye atakuwa nguvu kwao walindao langoni. |
Na Israeli wote wakapata habari za hukumu ile aliyoihukumu mfalme wakamwogopa mfalme; maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake, ili afanye hukumu.
Akaweka makamanda wa vita juu ya watu, akawakusanya kwake uwandani penye lango la mji, akawatia moyo; akisema,
kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo BWANA, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Na kivuli wakati wa joto; Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.
Na wakuu wa Yuda watasema mioyoni mwao, Wenyeji wa Yerusalemu wana nguvu katika BWANA wa majeshi, Mungu wao.
Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu; kwa sababu hamtoi Roho kwa kipimo.
Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenituma.
Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.
Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.