Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.
Hosea 14:1 - Swahili Revised Union Version Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Enyi Waisraeli, mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mmejikwaa kwa sababu ya uovu wenu. Biblia Habari Njema - BHND Enyi Waisraeli, mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Mmejikwaa kwa sababu ya uovu wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Samaria wataadhibiwa kwa kosa lao. Kwa sababu wamemwasi Mungu wao. Watauawa kwa upanga, vitoto vyao vitapondwapondwa, na kina mama wajawazito watatumbuliwa. Neno: Bibilia Takatifu Rudi, ee Israeli, kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa anguko lako! Neno: Maandiko Matakatifu Rudi, ee Israeli, kwa bwana Mwenyezi Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako! BIBLIA KISWAHILI Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako. |
Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.
Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.
Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Kama ukitaka kurudi, Ee Israeli, asema BWANA, utanirudia mimi; na kama ukitaka kuyaondoa machukizo yako, yasiwe mbele ya macho yangu, ndipo hutaondolewa;
Na dada yako mkubwa ni Samaria, akaaye mkono wako wa kushoto, yeye na binti zake; na dada yako mdogo, akaaye mkono wako wa kulia, ni Sodoma na binti zake.
Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Tena, japo ninamwambia mtu mwovu, Hakika utakufa; kama akighairi, na kuiacha dhambi yake, na kutenda yaliyo halali na haki;
Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.
Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi.
Haya ndiyo maangamizo yako, Ee Israeli, kwa kuwa wewe u kinyume changu mimi, kinyume cha msaada wako.
Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; kwa sababu hiyo, Israeli na Efraimu watajikwaa katika uovu wao. Yuda naye atajikwaa pamoja nao.
Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.
Efraimu amepandwa mahali pazuri, kama nilivyoona Tiro; lakini Efraimu atamtolea mwuaji watoto wake.
Siku za kupatilizwa zimekuja, siku za kulipa zimefika; Israeli atayajua hayo; huyo nabii ni mpumbavu, huyo mtu mwenye roho ana wazimu; kwa sababu ya wingi wa uovu wako, na kwa sababu uadui umekuwa mkubwa.
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;