Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Amosi 1:13 - Swahili Revised Union Version

13 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi, waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi, waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Amoni wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Katika vita vyao vya kupora nchi zaidi, waliwatumbua wanawake waja wazito nchini Gileadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu: “Kwa dhambi tatu za Amoni, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi ili kuongeza mipaka yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hili ndilo asemalo bwana: “Kwa dhambi tatu za Amoni, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi ili kuongeza mipaka yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;

Tazama sura Nakili




Amosi 1:13
27 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno, na sululu za chuma, na mashoka ya chuma, akawafanyiza kazi tanurini mwa matofali; ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni. Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu.


Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua.


Naye BWANA akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.


Hazaeli akasema, Bwana wangu analilia nini? Akajibu, Kwa sababu nayajua mabaya utakayowatenda wana wa Israeli; utazichoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, utawasetaseta watoto wao wachanga na wanawake wao wenye mimba utawapasua.


Baada ya hayo, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani.


Na sasa, tazama, wana wa Amoni, na Moabu, na wa mlima Seiri, ambao hukuwaacha Israeli waingie katika nchi yao, walipotoka nchi ya Misri; lakini wakawageukia mbali, wasiwaharibu;


Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?


Gebali, na Amoni, na Amaleki, Na Filisti, nao wanaokaa Tiro,


Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hadi ikawa hapana nafasi tena, nanyi ikawa hamna budi kukaa peke yenu katikati ya nchi!


Edomu, na Moabu, na wana wa Amoni;


Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Kwa sababu umesema, Mataifa haya mawili na nchi hizi mbili zitakuwa zangu, nasi tutazimiliki, ijapokuwa BWANA alikuwako huko.


Samaria atachukua hatia yake; kwa maana amemwasi Mungu wake; wataanguka kwa upanga; watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande, na wanawake wao wenye mimba watatumbuliwa.


Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma;


na utakaposongea kuwaelekea wana wa Amoni, usiwasumbue wana wa Amoni, wala usishindane nao; kwa kuwa sitakupa katika nchi ya hao wana wa Amoni kuwa milki yako; kwa sababu nimewapa wana wa Lutu iwe milki yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo