Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 19:22 - Swahili Revised Union Version

22 Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Mwenyezi-Mungu atawaadhibu Wamisri na kuwaponya. Nao watamrudia, naye atayasikiliza maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Mwenyezi-Mungu atawaadhibu Wamisri na kuwaponya. Nao watamrudia, naye atayasikiliza maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Mwenyezi-Mungu atawaadhibu Wamisri na kuwaponya. Nao watamrudia, naye atayasikiliza maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Mwenyezi Mungu ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Mwenyezi Mungu, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 bwana ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia bwana, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

22 Naye BWANA atapiga Misri, akipiga na kuponya; nao wakirudi kwa BWANA, atakubali maombi yao na kuwaponya.

Tazama sura Nakili




Isaya 19:22
21 Marejeleo ya Msalaba  

Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, BWANA, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa BWANA.


Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.


Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.


Kisha hao vyura watakwea juu yako wewe, na juu ya watu wako, na juu ya watumishi wako wote.


Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.


Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.


Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.


BWANA asema hivi, Kazi ya Misri, na bidhaa ya Kushi, na Waseba, watu walio warefu, watakujia, nao watakuwa wako; watakufuata; watakuja katika minyororo; wataanguka chini mbele yako, watakuomba, wakisema, Hakika Mungu yu ndani yako; wala hapana mwingine, hapana Mungu tena.


Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.


Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.


Zifanye akili za watu hawa zipumbae, na uyatie uzito masikio yao, na uyafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.


Maana Bwana MUNGU asema hivi; Mwisho wa miaka arubaini nitawakusanya Wamisri, na kuwatoa katika hayo makabila ya watu, ambazo walitawanyika kati yao;


Ee Israeli, mrudie BWANA, Mungu wako; maana umeanguka kwa sababu ya uovu wako.


Nitakwenda zangu niparudie mahali pangu, hata watakapoungama makosa yao na kunitafuta uso wangu; katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.


Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.


Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,


Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoeshwa nayo matunda ya haki yenye amani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo