Hosea 13:14 - Swahili Revised Union Version Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma! Biblia Habari Njema - BHND Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma! Neno: Bibilia Takatifu “Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee Kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma, Neno: Maandiko Matakatifu “Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma, BIBLIA KISWAHILI Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu. |
Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.
Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.
Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Umenikataa mimi, asema BWANA, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.
Mtu huyo na awe kama miji ile, ambayo BWANA aliiangamiza, asijute; na asikie kilio asubuhi, na kelele za fujo adhuhuri;
BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;
Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi.
Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia BWANA, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.
Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?
Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.
Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.