Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 13:14 - Swahili Revised Union Version

14 Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Yanibidi kuwakomboa hawa watu kutoka kuzimu; sharti niwaokoe kutoka kifoni! Ewe Kifo, yako wapi maafa yako? Ewe Kuzimu, yako wapi maangamizi yako? Mimi sitawaonea tena huruma!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 “Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee Kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 “Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.

Tazama sura Nakili




Hosea 13:14
32 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo amwoneapo rehema, na kusema, Mwokoe asishuke shimoni; Mimi nimeuona ukombozi.


Katika shingo yake hukaa nguvu, Na utisho hucheza mbele yake.


Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.


Umeniinua nafsi yangu, Ee BWANA, kutoka kuzimu. Umenihuisha na kunitoa Miongoni mwao washukao Shimoni.


Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu, Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanipokea.


Usiogope mtu atakapopata utajiri, Na fahari ya nyumba yake itakapoongezeka.


Wewe, uliyetuonesha mateso mengi, mabaya, Utatuhuisha tena. Utatupandisha juu tena Kutoka katika vina virefu chini ya nchi.


Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.


Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.


Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.


Umenikataa mimi, asema BWANA, umerudi nyuma; ndiyo maana nimenyosha mkono wangu juu yako, na kukuangamiza; nimechoka kwa kughairi.


Mtu huyo na awe kama miji ile, ambayo BWANA aliiangamiza, asijute; na asikie kilio asubuhi, na kelele za fujo adhuhuri;


BWANA asema hivi, awapaye watu jua, ili kuwa nuru wakati wa mchana, na amri za mwezi na nyota, ili kuwa nuru wakati wa usiku, aichafuaye bahari, hata mawimbi yake yakavuma; BWANA wa majeshi, ndilo jina lake;


Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi.


Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, nasi tutaishi mbele zake.


Na kiburi cha Israeli chamshuhudia mbele ya uso wake; ila hata hivyo hawakumrudia BWANA, Mungu wao, wala hawakumtafuta kwa ajili ya hayo yote.


Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.


Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?


Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?


Kwa sababu karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.


Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.


atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.


Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.


Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.


Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa wanyama wa nchi.


Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo