Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Hesabu 4:49 - Swahili Revised Union Version

Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kila mmoja alipewa kazi yake ya kufanya kuhusu kubeba hema la mkutano, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa amri ya Mwenyezi Mungu kupitia Musa, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa amri ya bwana kupitia Musa, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba. Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kama bwana alivyomwamuru Musa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa amri ya BWANA, walihesabiwa kwa mkono wa Musa, kila mtu kwa utumishi wake, na kama mzigo wake ulivyokuwa; ndivyo walivyohesabiwa na yeye, kama BWANA alivyomwagiza Musa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Hesabu 4:49
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Walawi kwa kulifuata kabila la baba zao hawakuhesabiwa katika watu hao.


Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


Lakini Walawi hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli; kama BWANA alivyomwagiza Musa.


kisha hizo fedha za ukombozi Musa akampa Haruni na wanawe, kama neno la BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Na Haruni na wanawe watakapokwisha kupafunika mahali patakatifu, na vyombo vyote vya mahali patakatifu, hapo watakapong'oa kambi; baadaye, wana wa Kohathi watakuja kuvichukua; lakini wasiviguse vile vitu vitakatifu, wasife. Vyombo vile ni mzigo wa wana wa Kohathi katika hema ya kukutania.


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,


Huu ni utumishi wa jamaa za Wagershoni, katika kutumika na katika kuchukua mizigo;


Na mausia ya mzigo wao ni haya, kwa utumishi wao wote katika hema ya kukutania; mbao za Hema Takatifu, na mataruma yake, na nguzo zake, na vitako vyake;


na viguzo vya ua vya kuuzunguka pande zote, na vitako vyake, na vigingi vyake, na kamba zake, na vyombo vyake vyote, pamoja na utumishi wake wote; nanyi mtawaagizia kila mtu kwa jina lake vile vyombo vya mzigo wao watakaoulinda.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za Wakohathi, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA kwa mkono wa Musa.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Gershoni, wote waliotumika katika hema ya kukutania, ambao Musa na Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA.


Hao ndio waliohesabiwa katika jamaa za wana wa Merari, ambao Musa na; Haruni waliwahesabu kwa amri ya BWANA, kwa mkono wa Musa.


Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,