Hesabu 3:21 - Swahili Revised Union Version Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Familia za Walibni na Washimei zilitokana na Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagershoni. Biblia Habari Njema - BHND Familia za Walibni na Washimei zilitokana na Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagershoni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Familia za Walibni na Washimei zilitokana na Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa jamaa za Wagershoni. Neno: Bibilia Takatifu Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizo zilikuwa koo za Wagershoni. Neno: Maandiko Matakatifu Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni. BIBLIA KISWAHILI Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni. |
Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni, na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao.
Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu.
Na wana wa Merari kwa jamaa zao ni Mahli, na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kwa nyumba za baba zao.
Hao waliohesabiwa kwao, kama hesabu ya wanaume wote, kuanzia umri wa mwezi mmoja na zaidi, hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu saba na mia tano.
Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.