Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Hesabu 24:4 - Swahili Revised Union Version Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu, mtu anayesujudu na kuona wazi. Biblia Habari Njema - BHND kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu, mtu anayesujudu na kuona wazi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kauli ya mtu aliyesikia maneno ya Mungu mtu aliyeona maono ya Mungu Mwenye Nguvu, mtu anayesujudu na kuona wazi. Neno: Bibilia Takatifu ujumbe wake yeye anayesikia maneno ya Mungu, anayeona maono kutoka kwa Mwenyezi, ambaye husujudu, na macho yake yamefunguka: Neno: Maandiko Matakatifu ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu, ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi, ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka: BIBLIA KISWAHILI Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho; |
Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.
Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia.
Akasema, Niliwaona Waisraeli wote wametawanyika milimani, kama kondoo wasio na mchungaji. BWANA akasema, Hawa hawana bwana; na warudi kila mtu nyumbani kwake kwa amani.
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu.
Kama kuonekana kwa upinde wa mvua, ulio katika mawingu siku ya mvua, ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwa mwangaza ule pande zote. Ndivyo kulivyokuwa kuonekana kwake mfano huo wa utukufu wa BWANA. Nami nilipoona nilianguka kifudifudi, nikasikia sauti ya mmoja anenaye.
Kisha akawaambia, Sikilizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, BWANA, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.
Mungu akamjia Balaamu usiku, akamwambia, Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita, nenda pamoja nao; lakini neno lile nitakalokuambia ndilo utakalolitenda, basi.
Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, akiwa na upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa, naye akainamisha kichwa, akaanguka kifudifudi.
Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema,
Na Petro alikuwa akiyafikiri yale maono. Roho akamwambia, Wako watu watatu wanakutafuta.
Ikawa nilipokwisha kurudi Yerusalemu, nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, nikawa katika hali ya kuzimia roho,
Nilikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Nami nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho,
Naye akavua nguo zake, akatabiri mbele ya Samweli, akalala uchi mchana kutwa na usiku kucha siku ile. Kwa hiyo watu wakasema, Je! Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?