Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Ezra 10:5 - Swahili Revised Union Version

Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Waisraeli wote, ya kwamba watafanya hivyo. Basi wakaapa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ezra alianza kwa kuwafanya makuhani, viongozi, Walawi na Waisraeli wengine wote waape kwamba watafanya kama ilivyosemwa, nao wakakubali kula kiapo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ezra alianza kwa kuwafanya makuhani, viongozi, Walawi na Waisraeli wengine wote waape kwamba watafanya kama ilivyosemwa, nao wakakubali kula kiapo.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ezra alianza kwa kuwafanya makuhani, viongozi, Walawi na Waisraeli wengine wote waape kwamba watafanya kama ilivyosemwa, nao wakakubali kula kiapo.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Waisraeli wote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Basi Ezra akainuka na kuwaapisha makuhani viongozi, Walawi na Israeli yote kufanya lile lililokuwa limependekezwa. Nao wakaapa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ndipo Ezra akaondoka, akawaapisha wakuu wa makuhani, na Walawi, na Waisraeli wote, ya kwamba watafanya hivyo. Basi wakaapa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Ezra 10:5
10 Marejeleo ya Msalaba  

Haya basi! Na tufanye agano na Mungu wetu, kuachana na wake zetu, na wale waliozaliwa nao, tukilifuata shauri la bwana wangu, na shauri la hao wanaoitetemekea amri ya Mungu wetu; mambo haya na yatendeke kwa kuifuata torati.


wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;


Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.


Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama walivyoahidi.


mwenye hekima asikie na kuongezewa elimu, na mwenye ufahamu ayafikie mashauri yenye njia.


Mtu hulifurahia jibu la kinywa chake; Na neno linenwalo wakati wa kufaa ni jema kama nini!


Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.


Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;


Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.