Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
2 Samueli 5:18 - Swahili Revised Union Version Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafilisti walifika na kujitawanya kwenye Bonde la Refaimu. Biblia Habari Njema - BHND Wafilisti walifika na kujitawanya kwenye Bonde la Refaimu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafilisti walifika na kujitawanya kwenye Bonde la Refaimu. Neno: Bibilia Takatifu Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, Neno: Maandiko Matakatifu Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, BIBLIA KISWAHILI Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai. |
Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.
Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.
Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
Yoshua akawaambia, Kwa kuwa wewe u taifa kubwa la watu, haya, kwea uende mwituni, ujikatie mahali hapo kwa ajili ya nafsi yako katika nchi ya Waperizi, na ya hao Warefai; maana hiyo nchi ya vilima ya Efraimu ni nyembamba, haikutoshi.
kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli,