Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 14:5 - Swahili Revised Union Version

5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, mfalme Kedorlaomeri na wale wafalme wenzake walikuja na kuwashinda watu wa Refaimu huko Ashtaroth-karnaimu, na Wazuzi huko Hamu, na Waemi huko Shawe-kiriathaimu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, mfalme Kedorlaomeri na wale wafalme wenzake walikuja na kuwashinda watu wa Refaimu huko Ashtaroth-karnaimu, na Wazuzi huko Hamu, na Waemi huko Shawe-kiriathaimu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, mfalme Kedorlaomeri na wale wafalme wenzake walikuja na kuwashinda watu wa Refaimu huko Ashtaroth-karnaimu, na Wazuzi huko Hamu, na Waemi huko Shawe-kiriathaimu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walienda vitani na wakawashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-Kiriathaimu,

Tazama sura Nakili




Mwanzo 14:5
28 Marejeleo ya Msalaba  

Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi.


na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai,


Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai.


Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.


Lakini wakapanda hao Wafilisti tena mara ya pili, wakajitawanya bondeni mwa Warefai.


Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka mwambani, wakamwendea Daudi, hadi pango la Adulamu; na jeshi la Wafilisti walikuwa wamefanya kambi bondeni mwa Warefai.


Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya katika bonde la Warefai.


Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.


Israeli naye akaingia Misri, Yakobo akawa mgeni katika nchi ya Hamu.


Akatenda mambo ya ishara zake kati yao, Na miujiza katika nchi ya Hamu.


Matendo ya ajabu katika nchi ya Hamu, Mambo ya kutisha penye Bahari ya Shamu.


Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu.


Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.


Kuhusu Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.


na juu ya Kiriathaimu, na juu ya Beth-gamuli, na juu ya Beth-meoni;


Na wana wa Reubeni wakajenga Heshboni, na Eleale, na Kiriathaimu;


alipokwisha kumpiga Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa akikaa Ashtarothi iliyo katika Edrei;


(Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).


na nchi ya Gileadi iliyobaki, na Bashani yote, maana huo ufalme wa Ogu niliwapa nusu ya kabila la Manase; nchi yote ya Argobu, nayo ndiyo Bashani yote. (Na nchi hii yaitwa nchi ya Warefai.


hata BWANA awapumzishe ndugu zenu kama ninyi, nao pia waimiliki nchi wapewayo na BWANA, Mungu wenu, ng'ambo ya Yordani; ndipo mtakaporudi kila mmoja aende katika milki yake niliyowapa.


Msiwache, kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye awapiganiaye.


tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,


ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.


na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde;


na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.


na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo