2 Samueli 23:6 - Swahili Revised Union Version Lakini hatawachipuza watu wasiofaa; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Maana haichukuliki kwa mkono, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini wasiomcha Mungu wote ni kama miiba inayotupwa tu, maana haiwezi kuchukuliwa kwa mkono; Biblia Habari Njema - BHND Lakini wasiomcha Mungu wote ni kama miiba inayotupwa tu, maana haiwezi kuchukuliwa kwa mkono; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini wasiomcha Mungu wote ni kama miiba inayotupwa tu, maana haiwezi kuchukuliwa kwa mkono; Neno: Bibilia Takatifu Lakini watu waovu wote watatupwa kando kama miiba, ambayo haikusanywi kwa mkono. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini watu waovu wote watatupwa kando kama miiba, ambayo haikusanywi kwa mkono. BIBLIA KISWAHILI Lakini hatawachipuza watu wasiofaa; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Maana haichukuliki kwa mkono, |
Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.
Mimi sina hasira ndani yangu; Kama mbigili na miiba ingekuwa mbele zangu, Ningepanga vita juu yake, Ningeiteketeza yote pamoja.
Na wewe, mwanadamu, usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao, ijapokuwa miiba na michongoma inakuzunguka, nawe unakaa katikati ya nge; usiyaogope maneno yao, wala usifadhaike kwa sababu ya nyuso zao, wajapokuwa ni nyumba yenye kuasi.
Mtu aliye mwema miongoni mwao ni kama mbigili; mtu aliye mwenye adili miongoni mwao ni mbaya kuliko boma la michongoma; hiyo siku ya walinzi wako, yaani, siku ya kujiliwa kwako, imefika; sasa kutatokea kufadhaika kwao.
Mwana wa Adamu atawatuma malaika wake, nao watakusanya kutoka katika ufalme wake machukizo yote, na hao watendao maasi,
Kumetoka katikati yako mabaradhuli kadha wa kadha, wamewapotoa wenyeji wa mji wao, wakisema, Twendeni tukaabudu miungu mingine msiyoijua;
Basi sasa ujue na kufikiri utakayotenda; kwa sababu yamekusudiwa mabaya juu ya bwana wetu, na juu ya nyumba yake yote; kwa kuwa yeye ni mtu asiyefaa kabisa, hata mtu hawezi kusema naye.