Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
1 Samueli 20:24 - Swahili Revised Union Version Basi Daudi akajificha shambani; na mwezi ulipoandama, mfalme aliketi kula chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Daudi akajificha shambani. Wakati wa sherehe za mwezi mwandamo, mfalme Shauli akaketi mezani kula. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Daudi akajificha shambani. Wakati wa sherehe za mwezi mwandamo, mfalme Shauli akaketi mezani kula. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Daudi akajificha shambani. Wakati wa sherehe za mwezi mwandamo, mfalme Shauli akaketi mezani kula. Neno: Bibilia Takatifu Basi Daudi akajificha shambani, na sikukuu ya Mwezi Mwandamo ilipowadia, mfalme akaketi ili ale. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Daudi akajificha shambani, na sikukuu ya Mwezi Mwandamo ilipowadia, mfalme akaketi ili ale. BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akajificha shambani; na mwezi ulipoandama, mfalme aliketi kula chakula. |
Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng'ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Na wakati mnapokula chakula na kunywa, je, Hamli kwa ajili ya nafsi zenu, na kunywa kwa ajili ya nafsi zenu?
Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
Na kwa habari ya neno lile tulilonena, wewe na mimi, angalia BWANA yu kati ya wewe na mimi milele.
Mfalme aliketi kitini mwake kama sikuzote, katika kiti kilichokuwa karibu na ukuta; Yonathani alikuwa mbele yake; Abneri naye akaketi karibu na Sauli; lakini mahali pake Daudi palikuwa hapana mtu.
Naye Daudi akamwambia Yonathani, Tazama, kesho ni mwandamo wa mwezi, nami hainipasi kukosa kuketi chakulani pamoja na mfalme; lakini niache nijifiche bondeni hadi siku ya tatu jioni.