Ndipo Farao akatuma watu kumwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao.
1 Samueli 2:8 - Swahili Revised Union Version Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Huwainua maskini toka mavumbini; huwanyanyua wahitaji toka majivuni, akawaketisha pamoja na wakuu, na kuwarithisha viti vya heshima. Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu; yeye ameisimika dunia juu ya minara yake. Biblia Habari Njema - BHND Huwainua maskini toka mavumbini; huwanyanyua wahitaji toka majivuni, akawaketisha pamoja na wakuu, na kuwarithisha viti vya heshima. Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu; yeye ameisimika dunia juu ya minara yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Huwainua maskini toka mavumbini; huwanyanyua wahitaji toka majivuni, akawaketisha pamoja na wakuu, na kuwarithisha viti vya heshima. Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu; yeye ameisimika dunia juu ya minara yake. Neno: Bibilia Takatifu Humwinua maskini kutoka mavumbini na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu; huwaketisha pamoja na wakuu, na kuwafanya warithi kiti cha utawala cha heshima. “Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya Mwenyezi Mungu; juu yake ameuweka ulimwengu. Neno: Maandiko Matakatifu Humwinua maskini kutoka mavumbini na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu; huwaketisha pamoja na wakuu na kuwafanya warithi kiti cha enzi cha heshima. “Kwa kuwa misingi ya dunia ni ya bwana; juu yake ameuweka ulimwengu. BIBLIA KISWAHILI Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. |
Ndipo Farao akatuma watu kumwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao.
Basi wewe utakuwa msimamizi wa nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.
Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;
Kwa kuwa mimi nilikuinua kutoka katika mavumbi, na kukufanya uwe mkuu juu ya watu wangu Israeli; nawe umeiendea njia ya Yeroboamu, na kuwakosesha watu wangu Israeli, hata wanighadhibishe kwa makosa yao;
Akainuka akaingia nyumbani; naye akayamimina yale mafuta kichwani mwake, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, yaani, juu ya Israeli.
akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vile vile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.
Lakini alimwinua mhitaji juu mbali na mateso, Na kuwaongeza jamaa zao kama kundi la kondoo.
Kwa maana anaweza kutoka gerezani kutawala; hata ikiwa alizaliwa akiwa maskini katika ufalme.
Nami nitamkaza kama msumari mahali palipo imara; naye atakuwa kiti cha utukufu kwa nyumba ya baba yake.
Basi mfalme akamtukuza Danieli, akampa zawadi kubwa nyingi sana, akamfanya kuwa mkubwa juu ya utawala wote wa Babeli, na kuwa mtawala mkuu juu ya wote wenye hekima wa Babeli.
Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye Juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.
Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na watawala, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kulia wa Ukuu huko juu;
Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.
Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Yeye ashindaye, nitamridhia kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.
Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.