Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hadi katika mlima Garebu, tena itazunguka na kufika Goa.
Zekaria 2:2 - Swahili Revised Union Version Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Naye akanijibu, “Ninakwenda kuupima urefu na upana wa mji wa Yerusalemu.” Biblia Habari Njema - BHND Basi, nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Naye akanijibu, “Ninakwenda kuupima urefu na upana wa mji wa Yerusalemu.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Naye akanijibu, “Ninakwenda kuupima urefu na upana wa mji wa Yerusalemu.” Neno: Bibilia Takatifu Nikamuuliza, “Unaenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” Neno: Maandiko Matakatifu Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.” BIBLIA KISWAHILI Ndipo nikasema, Unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. |
Na kamba ya kupimia itaendelea moja kwa moja hadi katika mlima Garebu, tena itazunguka na kufika Goa.
Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.
Nanyi mtaiandika milki ya mji, upana wake elfu tano, na urefu wake elfu ishirini na tano, kandokando ya mahali palipotolewa, iwe sehemu takatifu; nayo itakuwa ya nyumba yote ya Israeli.
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.
Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenituma, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwenda wapi?
Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wanaosujudu humo.