Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 1:16 - Swahili Revised Union Version

16 Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kwa hiyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, naurudia mji wa Yerusalemu kwa huruma; humo itajengwa nyumba yangu, na ujenzi mpya wa mji utaanza.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kwa hiyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, naurudia mji wa Yerusalemu kwa huruma; humo itajengwa nyumba yangu, na ujenzi mpya wa mji utaanza.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kwa hiyo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu, naurudia mji wa Yerusalemu kwa huruma; humo itajengwa nyumba yangu, na ujenzi mpya wa mji utaanza.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa juu ya Yerusalemu,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo bwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




Zekaria 1:16
24 Marejeleo ya Msalaba  

Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake – hakika unajua! Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?


Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.


Kozi na nungunungu wataimiliki, bundi na kunguru watakaa huko, naye atanyosha juu yake kamba ya ukiwa na timazi ya utupu.


BWANA asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.


Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.


Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, akielekea mashariki, akapima dhiraa elfu moja, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka katika vifundo vya miguu.


Kuuzunguka ni mianzi elfu kumi na nane; na jina la mji huo tangu siku hiyo litakuwa hili, BWANA yupo.


BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;


Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni BWANA, Mungu wao, nami nitawasikia.


naye akamwambia, Nenda mbio ukamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake.


Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.


Haya! Haya! Ikimbieni nchi ya kaskazini, asema BWANA; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema BWANA.


Mikono yake Zerubabeli imeiweka misingi ya nyumba hii, na mikono yake ndiyo itakayoimaliza; nawe utajua ya kuwa BWANA wa majeshi amenituma kwenu.


BWANA asema hivi, Mimi nimerudi Sayuni, nami nitakaa katikati ya Yerusalemu; na Yerusalemu utaitwa, Mji mwaminifu; na mlima wa BWANA wa majeshi utaitwa, mlima mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo