Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda.
Zekaria 12:13 - Swahili Revised Union Version jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Shimei peke yake. Biblia Habari Njema - BHND ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Shimei peke yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza ukoo wa Lawi peke yake na ukoo wa Shimei peke yake. Neno: Bibilia Takatifu ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, Neno: Maandiko Matakatifu ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, BIBLIA KISWAHILI jamaa ya nyumba ya Lawi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Shimei peke yao, na wake zao peke yao. |
Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda.
Ila Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Nathani, nabii, na Shimei, na Rei, na mashujaa wa Daudi, hao hawakuwa pamoja na Adonia.
Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.
Na wana wa Pedaya; Zerubabeli, na Shimei; na wana wa Zerubabeli; Meshulamu na Hanania; na Shelomithi alikuwa dada yao;
Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; lakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kama wana wa Yuda.
Nayo nchi itaomboleza, kila jamaa peke yake; jamaa ya nyumba ya Daudi peke yao, na wake zao peke yao; jamaa ya nyumba ya Nathani peke yao, na wake zao peke yao;
Na wana wa Merari kwa jamaa zao ni Mahli, na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kwa nyumba za baba zao.
Katika Gershoni walikuwa jamaa ya Walibni, na jamaa ya Washimei, hawa ndio jamaa za Wagershoni.